Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG, Lule kuna kitu

Luleeeeeee Singida FG, Lule kuna kitu

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Uongozi wa Singida Big Stars umeachana kimyakimya na aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho, Mathias Lule ikiwa ni mwezi mmoja tangu klabu hiyo iingie mkataba na kocha Mbrazili, Ricardo Ferreira kuchukua nafasi ya Ernst Middendorp.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Uganda, Lule aliliambia Mwanaspoti ni kweli ameondoka ndani ya kikosi hicho ila mambo mengine ya kilichomuondoa asingependa kuyaweka wazi kwa sababu anaheshimu uamuzi uliofanyika na kufikiwa baina yao.

“Nimeondoka Singida na kwa sasa nimerudi nyumbani Uganda, kama nilivyosema mwanzo nisingependa kuelezea sababu binafsi kwa sababu suala la kocha kuondoka sehemu moja na kwenda nyingine ni la kawaida kwani ndio kazi zetu zilivyo,” alisema.

Ofisa Habari wa Singida, Hussein Massanza alipotafutwa na Mwanaspoti kuzungumzia suala hilo alisema Lule bado ni kocha wao na wana mkataba naye hivyo jambo la kuachwa halitambui na yupo ndani ya timu kuendelea na majukumu.

“Mimi ninachojua kocha Lule bado yupo Tanzania na anaendelea na majukumu yake kama kawaidia hivyo hizo habari za kusema kaenda kwao Uganda mimi sizijui kwa kweli, tunachokifanya ni kuendelea na maandalizi yetu ya michezo ijayo,” alisema.

Hata hivyo, wakati Massanza anazungumza hayo Mwanaspoti linatambua kocha huyo ameondoka na hayupo nchini kutokana na kocha mpya wa kikosi hicho, Ferreira kuleta wasaidizi wake anaoamini watakuwa na manufaa kuiletea timu hiyo mafanikio.

Chanzo: Mwanaspoti