Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG Kambi Dar wakisaka Makundi Shirikisho Afrika

Singida FG DAR Singida FG kuweka Kambi Dar wakisaka Makundi Shirikisho

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Singida Fountain Gate imeanza safari kwenda Dar es Salaam ikitokea mkoani Singida kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kwanza (first leg) hatua ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Future FC ya Misri Septemba 17 mwaka huu katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Kabla ya kuivaa Future FC timu hiyo itacheza michezo ya kirafiki ukiwemo ule wa kimataifa dhidi ya Arta Solar 7 ya Djibouti utakaochezwa Septemba 7 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru.

Hata hivyo Singida itakwenda kuanza michezo yao ya kirafiki na kimataifa wakiwa na benchi jipya la ufundi likiongozwa na kochaa mkuu Ernest Middendrorp baada ya Hans Van Puljin kubwaga manyanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live