Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG, JKT hakuna mbabe Uwanja wa Liti

IMG 6372.jpeg Singida FG, JKT hakuna mbabe Uwanja wa Liti

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Singida Fountain Gate imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa LITI mjini Singida.

Mabao ya Singida Fountain Gate yamefungwa na Marouf Tchakei dakika ya 62 na Francy Kazadi dakika ya 75, wakati ya JKT Tanzania yamefungwa na Hassan Kapalata dakika ya 26 na Hassan Nassor Maulid dakika ya 68.

Kwa matokeo hayo, Singida Fountain Gate inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya nne, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 16 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live