Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida F.G yafafanua uwepo wa Manyika

Peter Manyika Sngida FG Singida F.G yafafanua uwepo wa Manyika

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Singida Fountain Gate umeeleza kuwa umemuongeza kocha wa makipa, Manyika Peter kwenye benchi lao kutokana na uzoefu mkubwa alionao ili kuziba nafasi ya kocha Moses Temba.

Ofisa Habari wa Singida, Hussein Masanza amesema wamemchukua Manyika baada ya Temba kuhitajika kwenda kuongeza elimu yake.

“Tumemchukua Manyika kutokana na uzoefu alionao na historia kubwa kuhusu soka nchini, hivyo tunatarajia uzoefu wake kutusaidia mno kwa kipindi hiki wakati kocha Temba ameenda kuongeza elimu ya leseni C kutoka leseni D aliyonayo sasa,” amesema Masanza.

Manyika kipa wa zamani wa Taifa Stars na Young Africans, alionekana kwenye benchi la timu hiyo kwa mara ya kwanza katika mchezo wa mwisho wa ligi ambao Singida ilifungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Liti, Singida.

Aidha, Masanza amesema kuhusu kocha mkuu mpya wa timu hiyo baada ya Emst Middendorp kuondoka, suala hilo bado linafanyiwa kazi licha ya kuelezwa kati ya Pablo Franco au Didier Gomes waliowahi kuinoa Simba SC, mmojawapo anatarajiwa kurithi kibarua hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live