Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Black Stars: Tumeshamlipa Israel Mwenda, tunataka aje kambini haraka

Mwenda Mszz Beki Israel Patrick Mwenda

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars unapenda kuwajulisha wadau na mashabiki wetu kuwa tumeona taarifa zinazosambaa kuhusu maslahi ya mchezaji wetu Israel Patrick Mwenda tuliyemsajili msimu huu 2024/2025 kwa Ada ya TZS milioni 200.

Makubaliano ya mkataba yaliweka kiasi cha pesa kinachotakiwa kulipwa kabla ya mchezaji kusaini ni TZS milioni 140 ambacho klabu ilimlipa kama mkataba ulivyotaka, kiasi kingine kilichobaki TZS milioni 60 kinatakiwa kulipwa muda wowote baada ya kukamilisha usajili.

Huu ni utaratibu wetu kama Klabu na wapo wachezaji wengine waliopewa malipo ya utangulizi kabla ya kusaini na malipo mengine wanaendelea kupokea wakiwa wanaendelea na Ligi.

Kuna wachezaji wamepokea malipo ya awali 20%, wengine 40% wengine 50%. Israel Mwenda amepokea milioni 140 kama kiambatisho kinavyoonesha na anadai milioni 60. Yeye amechagua kusubiri mpaka alipwe kwanza ndio ajiunge na timu tofauti na wenzake ambao wanalipwa huku wakiwa kazini kama ilivyo kwenye vilabu vingi hapa nchini.

Klabu itaendelea kufanyia kazi maslahi yake kwa mujibu wa makubaliano kwa kumalizia sehemu ya ada yake ya uhamisho iliyobaki ambayo inatakiwa kulipwa muda wowote baada ya kukamilisha usajili wake na mchezaji kujiunga rasmi na timu yetu.

Uongozi wa klabu unamtaka mchezaji kuripoti kambini haraka kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayoendelea kwa kuwa mahitaji yaliyobaki hayakuwa takwa la mkataba kuwa alipwe kwanza ndio aungane na timu kambini.



Chanzo: www.tanzaniaweb.live