Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars yapata ahueni

METACHA.png Mlinda mlango wa Singida Big Stars, Metacha Mnata

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mara baada ya kumaliza adhabu makipa wa timu ya Singida Big Stars (SBS) Metacha Mnata na Benedict Haule wamejiunga na wenzao kujiandaa na michezo inayofuata Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC na Ruvu Shooting.

Metacha alifungiwa michezo mitatu na faini ya Sh 1 milioni, alikosa michezo dhidi ya Polisi Tanzania, Simba na Yanga huku Haule akikosa miwili dhidi ya Simba na Yanga.

Sababu za kufungiwa Metacha ni kutokana na kuonesha utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kumkanyaga mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Charles Ilamfya.

Haule alipewa adhabu hiyo kutokana na kupata kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliofanyika Uwanja wa Black Rhino, Karatu. Mchezo huo ulimalizika SBS ikishinda bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.

Katika michezo hiyo Kocha Hans Van Pluijm alikuwa akimwanzisha kipa wa zamani wa Geita Gold, Abubakary Khomeiny ambaye ameruhusu mabao matano kwenye michezo mitatu aliyodaka.

SBS inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 18, ikicheza mechi 11 hadi sasa.

Msemaji wa SBS, Hussein Masanza alisema wachezaji hao wamejiunga na wenzao kwa ajili ya kujiandaa na michezo inayofuata Novemba 23 na 26 dhidi ya KMC na Ruvu Shooting.

Chanzo: Mwanaspoti