Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars yapania Mapinduzi Cup

Singida Big Mapinduzi Kikosi cha Singida Big Stars kikiendelea kujifua

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

SINGIDA Big Stars (SBS) imejipanga kufanya vizuri kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup yatakayoanza Januari Mosi hadi 13 kisiwani Unguja, Zanzibar.

Jumla ya timu 12 zinatarajia kushiriki mashindano hayo huku ikiwa mara ya kwanza kwa SBS kupata mwaliko huo.

Timu zinazoshiriki ni mabingwa watetezi Simba ambao waliuchukua ubingwa kwa kuwafunga Azam FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali,Y anga, Azam, Namungo na Azam.

Kwa upande wa Zanzibar timu zitakazoshiriki ni AVZ, Malindi, KMKM za Unguja na Chipukizi na Jamhuri za Pemba,pamoja na timu kutoka Burundi.

Msemaji wa timu hiyo, Hussein Massanza alisema wameupokea kwa mikono miwili mwaliko waliopewa na waandaaji wa mashindano hayo.

Alisema wanaendelea kujipanga kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kwenda kufanya vizuri katika mshindano hayo.

Kuhusu maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, msemaji huyo alisema wanaendelea na mazoezi na wanataka kupata pointi nyingi ili kujiweka katika nafasi nzuri.

Nahodha wa kikosi hicho, Deus Kaseke alisema wamejipanga mzunguko wa pili kupata pointi zaidi ya zile za mzunguko wa kwanza.

“Ligi ni ngumu na inaenda kuwa ngumu zaidi sisi tutaendelea kupambana katika mzunguko wa pili tupate pointi zaidi,” alisema Kaseke ambaye amewahi kuzichezea Mbeya City na Yanga. SBS imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ikishika nafasi ya 4 kwa kujikusanyia pointi 27 huku Yanga ikiongoza kwa kuwa na pointi 38 na Azam ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 35.

Chanzo: Mwanaspoti