Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars yamlilia kinda aliyefia uwanjani

Afariki Dogo Mohammed maarufu Banda amefariki mazoezi

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Uongozi wa Singida Big Stars umesema mchezaji wa timu hiyo aliyefariki mazoezi ni mwenyeji wa Kijiji cha Mlandala Kata ya Urughu wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Banda alifariki mapema leo asubuhi wakati timu SBS ya vijana ya U17 ikifanya mazoezi katika uwanja wa Magereza mkoani Singida.

Msemaji wa timu hiyo Hussein Massanza amesema marehemu ni mwenyeji wa Kijiji Cha Mlandala na alikuwa akiishi katika kempu ya timu hiyo.

Amesema wamewasiliana na familia ya mchezaji huyo na wanasubiria maelekezo kutoka kwao.

"Kama timu tumehuzunika na tupo pamoja katika kipindi hichi kigumu," amesema Msemaji.

Chanzo: Mwanaspoti