Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars yafungiwa na FIFA kufanya usajili, Kisa ni hiki..!

Pascal Wawa Serge Singida Big Stars yafungiwa na FIFA kufanya usajili, Kisa ni hiki..!

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limeifungia klabu ya Singida Fountain Gate FC kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Pascal Serge Wawa baada ya nyota huyo raia wa Ivory Coast kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Wawa alifungua kesi FIFA akidai malipo ya ada ya usajili (sign on fee) na malimbikizo ya mishahara huku klabu hiyo ikitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Taarifa ya Shirikisho la soka Tanzania TFF imesema “Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.”

“TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live