Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars wapanga kuibomoa Simba SC

Manula X Beno Kakolanya Magolikipa wa Simba, Beno Kakolanya na Aishi Manula

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Singida Big Stars kinasema, klabu hiyo imeanza mipango ya kumng’oa kipa Beno Kakolanya kutoka Simba ambaye mkataba wake unaelekea mwishoni kwa lengo la kumsajili aitumikie Timu hiyo kuanzia msimu ujao.

Mkataba wa Kakolanya na Simba unaisha mwishoni mwa msimu huu na hadi sasa inadaiwa hakuna makubaliano ya kusaini dili jipya licha ya mabosi wa Msimbazi kuzungumza naye hivi karibuni.

Mazungumzo baina ya Singida na Kakolanya yamefikia pazuri na muda wowote baada ya kurejea kutoka Misri anaweza kumwaga wino.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live