Kikosi cha Singida Big stars kimetonesha kidonda walichonacho KMC kuelekea mchezo wa ligi kuu kesho kwenye Dimba la Uhuru baada ya kutamba kwamba wamekuja kwa ajili ya kuchukua alama tatu.
Mchezaji wa Singida Big Stars Hamis Tambwe amesema malengo yao ni kumaliza kwenye nafasi tatu za juu kwenye ligi kuu Tanzania bara.
“Tulikuwa na malengo mawili, lengo la kwanza ni kumaliza kwenye nafasi nne za juu ili kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao na la pili ni hili la kutaka kumaliza nafasi ya tatu, Kmc watusamehe bure” Alisema Tabwe
Kwa upande wake kocha msaidizi wa Kmc Khalid Adam amesema wanauhitaji mno mchezo huo kwani umebeba hatma yao ya kubaki salama kwenye ligi kuu kwa msimu ujao.
“Tunafahamu tupo katika hali ngumu, lakini tutahakikisha tunapambana ili kusogea katika mazingira salama kwenye ligi” Alisema kocha Khalid Adam.
KMC wapo katika nafasi ya 14 wakiwa na alama 26 baada ya kushuka dimbani mara 27 na wanapambana ili kusalia kwenye ligi kwa msimu ujao.