Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars waishushia kipigo kizito Azam FC Mapinduzi Cup

Singida To Final.jpeg Singida Big Stars waishushia kipigo kizito Azam FC Mapinduzi Cup

Sun, 8 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Singida Big Stars imetinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Pongezi kwa mshambuliaji mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Francis Kazadi Kasengu aliyefunga mabao yote manne dakika za 27, 53, 64 na 86, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji Chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 43.

Sasa Singida Big Stars itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya Mlandege ya Zanzibar na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi.

Kasengu (30), ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa aliyeanzia kuwika AS Vita, DC Motema Pembe za kwao, SCC Mohammédia na Wydad Casablanca za Morocco na Al Masry SC ya Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live