Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars waichapa Polisi Tz, Kagere atuma salamu

Singida Big Star.jpeg Singida Big Stars waliibuka na ushind wa goli 1-0

Sun, 6 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Singida Big Stars imeendeleza wimbi la Ushindi baada ya leo kuifunga klabu ya Polisi Tanzania katika mchezo uliopigwa katika dimba la Black Rhino wilayani Karatu mkoani Manyara.

Singida Big Stars wanapata ushindi wao wa pili mfululizo baada ya kuifunga Polisi leo kwa bao 1-0 Goli lililowekwa kimiani na mshambualiaji wa zamani wa klabu ya Simba Meddie Kagere katika dakika ya 22 ya mchezo.

Walima alizeti hao wakiwa ugenini wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu na kusogea hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 17 kwenye michezo tisa waliyocheza.

Klabu ya Singida Big Stars ni miongoni mwa timu ambazo zilitarajiwa kuleta ushindani mkubwa kunako ligi ya NBC na ndicho wanachokifanya hivi sasa, Hiyo imekuja baada ya kulingana alama na Simba na Azam huku wakishika nafasi ya nne kwenye msimamo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live