Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars waichapa Namungo 3-0

Singida Big Starz Liti Wachezaji wa Singida Big Stars wakishangilia goli la Ndemla

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Singida Big Stars wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Disemba 2 Uwanja wa LITI mjini Singida.

Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na kiungo mzawa, Said Hamisi Ndemla dakika ya 28 na washambuliaji Mnyarwana, Meddie Kagere dakika ya 65 na Mrundi, Amissi Tambwe dakika ya 90 na ushei.

Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 27, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Namungo inabaki na pointi zake 18 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live