Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars kung'oa beki Prisons

Beki Prisonsssss.png Singida Big Stars kung'oa beki Prisons

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kujihakikishia nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa uongozi wa Singida Big Stars umeanza kujiimarisha baada ya kumalizana na beki namba mbili wa Tanzania Prisons, Ibrahim Abraham.

Abraham ni zao la timu hiyo ambaye wamempandisha kutoka timu ya vijana na tayari tangu amepandishwa ameonyesha ubora kwa kucheza mechi 22 za msimu huu hadi sasa wakiwa wamebakiza mechi mbili kumaliza msimu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya SBS kililiambia gazeti hili kuwa tayari wamemalizana na beki huyo ambaye amemvutia kocha Hans van Pluijm ambaye ameikubali uwezo wake.

"Ni pendekezo la kocha Hans van Pluijm amemhitaji akikiri kuwa ni beki mzuri ambaye anaweza kuisaidia SBS kwa miaka zaidi ya mitatu kutokana na umri wake huku akikiri kuwa ni mchezaji amzuri anaweza kumtumia kwenye nafasi tatu tofauti." kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti lilifanya jitihada za kumsaka beki huyo ambaye alikiri kupokea ofa kutoka SBS huku akiweka wazi kuwa ni mchezaji huru kwani mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

"Siwezi kusema mazungumzo yetu yamefikia wapi hadi sasa hayo ni mambo yangu binafsi lakini ni kweli wamekuja mezani na wananihitaji kuhusu waajiri wangu pia wamefanya mazungumzo na mimi ya kutaka niendelee kuwatumikia kwa msimu ujao.

"Kilichopo sasa naangalia ni ofa gani itakuwa nzuri kwangu kwasababu nacheza soka ili nipate fedha, atakayefikia mahitaji yangu ndiye nitakayemtumikia msimu ujao sasa nazingatia mechi zilizobaki ili niweze kuiona timu yangu inatimiza malengo ya kucheza msimu ujao." alisema beki huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: