Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Big Stars kuliamsha rasmi

Singida Pic Singida Big Star

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Uongozi wa Singida Big Star (zamani DTB) umeanza rasmi mipango yao kwa ajili ya msimu wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, huku ukisema leo utatangaza rasmi kuanza zoezi lao la usajili, licha ya kuhusishwa na wachezaji kadhaa kutoka klabu nyingine.

Singida imepanda Ligi Kuu kutoka Ligi ya Championship na imetangaza itautumia Uwanja wa Liti (zamani Namfua) kama uwanja wao nyumbani ligi itakapoanza. Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Muhibu Kanu alisema wamepokea ripoti ya kocha mkuu, Ramadhan Nsanzurwimo na imeonesha wachezaji watakaosajiliwa na watakaoachwa msimu ujao.

"Baada ya kuipokea na kuichambua kwa kina Jumatatu ndio tunaanza usajili, tutasajili kwa matakwa ya kocha ambaye Bodi ya Wakurugenzi ndio wenye jukumu la kumchagua,"alisema. Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoani Singida (Sirefa) Hamisi Kitila alisema ujio wa timu hiyo ni fursa kubwa kwa vipaji na wafanyabiashara wa Mkoa huo. Kitila aliahidi kupitia Sirefa watahakikisha Klabu hiyo inafanya vizuri katika Ligi hiyo huku akizikaribisha timu zingine kutumia uwanja wa Liti kama uwanja wao wa nyumbani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz