Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida BS yatuma ujumbe mzito Jangwani

Singida Kimataifa Singida BS yatuma ujumbe mzito Jangwani

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Singida Big Stars umetuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao Yanga ambao watacheza nao mechi mbili katika mashindano mawili tofauti.

Mchezo wa kwanza ni ule wa Azam Sports Federation ambao ni hatua ya nusu fainali Mei 4 na ule wa pili unatarajiwa kuchezwa Mei 7, ambao utakuwa ni wa ligi zote zitachezwa Uwanja wa Liti.

Ipo wazi kwamba bingwa mtetezi wa taji la Azam Sports Federation ni Yanga aliyetwaa mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa hatua ya fainali.

Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza ameliambia Championi Jumatatu kuwa wanatambua uimara wa wapinzani wao lakini hawana hofu kutokana na maandalizi ambayo wamefanya.

“Tunatambua ubora wa wapinzani wetu Yanga lakini haina maana kwamba tunamashaka hapana ugumu wa ratiba unatufanya tuwe kwenye maandalizi mazuri ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu.

“Wachezaji wapo tayari na wanatambua kuhusu mchezo huo ukizinagatia tulianza kukata tiketi mapema kwenye mashindano haya tukawa tunajua mshindi kati ya Yanga ama Geita Gold huyo tutakutana naye.

“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kuelekea kwenye mechi zetu za Mei ambazo zitachezwa Uwanja wa Liti ni mara ya kwanza kwetu kucheza nusu fainali ya kombe hili tunahitaji kufika fainali na kutwaa taji,” alisema Masanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: