Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida BS vs Kagera Sugar kazi ipo leo

Singida Hj Singida BS vs Kagera Sugar kazi ipo leo

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja Singida Big Stars ikiwa mwenyeji wa Kagera Sugar.

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa CCM Liti mjini Singida.

Katika mchezo wa kwanza kati ya timu hizo uliofanyika Desemba 21, 2022 kwenye uwanja Kaitaba mjini Bukoba, Singida Big Stars iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1.

Singida Big Stars inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 37 baada ya michezo 19 wakati Kagera Sugar ina pointi 24 ikishika nafasi ya 8.

Januari 16 imepigwa michezo miwili ya ligi hiyo ambapo vinara wa ligi Yanga imejiimarisha kieleleni baada ya kuichapa Ihefu bao 1-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Nayo Azam imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Azam Complex.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live