Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida BS vs Coastal Union ngoma nzito

Singida Robo Fainali Azam Singida BS vs Coastal Union ngoma nzito

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpango kazi wa Kocha Mkuu wa Singaida Big Stars, Hans Pluijm kusepa na pointi tatu dhidi ya Coastal Union ulikwama baada ya kuambulia pointi moja.

Ikiwa ugenini baada ya dakika 90 Machi 12,2023 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Coastal Union 1-1 Singida Big Stars.

Ni mastaa wawili walipachika mabao kwenye mchezo huo ambapo kwa Coastal Union wao ni Greyson Gerald alipachika bao dakika ya 44.

Mwamba Bright Adjei aliweka mzani sawa dakika ya 74 na kuwafanya Singida Big Stars kusepa na pointi moja ugenini.

Matokeo hayo yanaifanya Singida Big Stars kufikisha pointi 48 huku wakiwa nafasi tatu na Coastal Union nafasi ya 13 pointi 26.

Singida Big Stars mbele ya Coastal Union imekusanya pointi moja kwa kuwa mchezo wa kwanza ikiwa Uwanja wa Liti ilipoteza pointi zote tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live