Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida BS: Tumepangwa kundi la kifo Kagame Cup

Singida Ihefuuuuuuuuuuuuu Singida BS.

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Singida Black Stars ikisema timu yao imepangwa katika kundi gumu kuelekea michuano ya Kombe la Kagame, Coastal Union wao wamefurahia ratiba ya michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Julai 9 hadi 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Coastal Union iko katika Kundi A na timu za Al Wadi ya Sudani, JKU FC (Zanzibar) na Dekefaha (Somalia), huku Singida Black Stars ikiangukia Kundi C lenye SC Villa ya Uganda, APR (Rwanda) na El Merriekh (Sudan).

Katibu Mkuu wa Coastal Union, Ayoub Omari, amesema wamefurahishwa na droo hiyo, haswa kupangwa kwenye kundi ambalo wanalimudu.

"Kundi tumelipokea kwa mikono miwili, ni saizi yetu kabisa na tunalimudu, naahidi tutawapa Watanzania burudani, hakuna mashaka tumejiandaa na mashindano hayo.

Hiki ni kipimo kwetu kuelekea katika michuano ya kimataifa, Kombe la Shirikisho Afrika, watu wataona tumejiandaa vipi kwenye michuano hiyo," alisema katibu hiyo.

Aliongeza tayari kikosi chao kimeingia kambini kujiandaa na michuano hiyo na akaahidi watafika mapema Dar es Salaam ili kupata muda wa wachezaji wake kupumzika kabla ya kinyang'anyiro hicho kuanza.

Naye Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, aliliambia gazeti hili wamepangwa katika kundi la kifo, hivyo wana kazi ya ziada.

"Kundi nimeliona, katika makundi yote letu ndiyo gumu, lakini tunakwenda kujiandaa ili kupambana. Ni kipimo sahihi kwetu kupima ubora na daraja letu kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu.

Kocha wetu Mkuu (Patrick Aussems), ameliona, na yeye ndiye aliyeshauri tushiriki kwa ajili ya kupanga mbinu zake na kuangalia aina ya wachezaji waliosajiliwa, ila ukweli hatuna matarajio makubwa kwenye michuano hii zaidi ya kuitumia kujenga kikosi," amesema Masanza alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live