Kua nyuma ya Simba na Yanga kwenye Ligi kuu sio bahati mbaya, Ni uwekezaji mkubwa uliofanyika.
Tayari wana tiketi ya kushiriki Shirikisho Msimu ujao, Ni matumaini yangu watafika makundi.
Kwasababu wanacheza vizuri na Wana wachezaji wengi waongoza njia ambao wameshafika hizo hatua.
1. Ennock Attah Agyei - Amecheza nusu fainali ya kombe la Shirikisho Africa akiwa na Horoya AC.
2. Meddie Kagere - Amecheza robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika akiwa na Simba SC.
3. Francy Kazadi - Amecheza fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika akiwa na AS Vita Club.
4. Pascal Wawa - Amecheza robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika akiwa na Simba SC.
5. Ibrahim Ajib amecheza robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika akiwa na Simba SC.
6. Amis Tambwe - Amecheza makundi ya Kombe la Shirikisho Africa akiwa na Yanga SC.
7. Deus Kaseke - Amecheza makundi ya Kombe la Shirikisho Africa akiwa na Yanga SC.
8. Nicolas Gyan - Amecheza robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika akiwa na Simba SC.
9. Said Ndemla - Amecheza robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika akiwa na Simba SC.
10. Juma Abdul - Amecheza makundi ya Kombe la Shirikisho Africa akiwa na Yanga SC.
Singida ipo mikono salama.