Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simu ya baba na ujumbe mzito Andambwile alivyotua Yanga

Andambwileee M0n.jpeg Aziz Andambwile.

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simu nyingi ziliita muda mchache baada ya kutambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Yanga lakini simu ya baba yake mzazi ndio ilikuwa na ujumbe mkubwa kwake.

Hiyo ni kauli ya Aziz Andambwile ambaye amejiunga na Yanga dirisha hili la usajili.

“Ilikuwa ndoto yangu kucheza Yanga, lakini baba yangu kanionya kupambania nafasi na kujichunga ili niweze kufikia malengo nafikiri ni wakati sahihi kwangu kunyanyua makwapa,” anasema Andabwile.

AUCHO NI DAKTARI HASWA Ni kiungo wa Yanga ambaye ataitumikia kwa msimu wa nne (2024/25) baada ya mitatu ya mwanzo kumalizika na kucheza kwa mafanikio makubwa akiipa timu hiyo ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo, ngao na kucheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika na robo fainali Ligi ya Mabingwa.

“Nimewaona viungo wengi wa kigeni na kupata nafasi ya kucheza nao timu moja na wengine wapinzani wangu kati ya hao wote navutiwa na Aucho ni mchezaji mzuri anaufanya mpira uonekane rahisi uwanjani. “Kiungo huyo ni mtu sana anarahisisha sana mpira anafanya majukumu yake kwa ufasaha kiwanjani nimekuwa nikimtazama na kujifunza mengi kwake apewe maua yake.” anasema Andambwile ambaye amesema pia anavutiwa na Yaya Toure kiungo wa zamani wa Man City na Barcelona. 

MUDATHIR, KAGOMA Soka lina aina nyingi ya kujifunza na kujitofautisha na wengi kuna ambao hawawezi kumwaga sifa kwa wachezaji wenzao kutokana na kucheza nafasi moja na wengine wana moyo wa kuweka ukweli kama ilivyo kwa Andambwile ambaye anakiri anakoshwa na Mudathir Yahya na Yusuph Kagoma ni wazawa.

“Mudathir Yahya na  Yusuph Kagoma ni wachezaji wazuri wote wana umuhimu wao kwenye kikosi kwa nyakati tofauti na wanaweza kucheza pamoja kutokana na kuwa bora kwa kushambulia na kukaba wana jicho la kuona pasi inatakiwa kwenda wapi.

“Kwenye kutofautisha siwezi kwasababu naona wote uchezaji wao upo sawa na wanaubora sawa ni miongoni mwa viungo wazawa ambao nawakubali na nimekuwa nikiwatazama,” anasema.

AMRUDISHA BRUNO BONGO Singida Big Stars kabla haijabadilisha jina ilibahatika kumsajili Mbrazir Bruno Gomes ambaye ametimka nchini kwao na kujiunga na timu ya Athletic Club baada ya kuitumikia timu hiyo msimu mmoja na nusu, Andambwile amefunguka ubora wa kiungo huyo huku akikiri kuwa bado alikuwa anahitajika Tanzania.

“Bruno huyu kila mmoja anafahamu ubora wake kwa sababu kacheza msimu mmoja hakumalizia wa pili lakini kaonyesha uwezo mzuri akicheza sambamba na fundi Marouf Tchakei hawa wote kwangu ni wachezaji bora niliowahi kucheza nao timu moja,” anasema Andabwile. SIRI YA KUPIGA PENATI

Huenda akawa mchezaji wa kuokoa jahazi ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo akitokea Singida si haba ni fundi wa kupiga penati kama ambavyo yeye mwenyewe anafunguka.

“Ili mchezaji uweze kupiga penati nzuri kwanza unahitajika kuwa na utulivu na kumsoma kipa wapi anakwenda kwasababu ukikaa kwa kutulia na kumuangalia unajua kabisa anakwenda wapi hiyo ndio siri ya ubora wa upigaji wa penati,” anasema kiungo huyo ambaye anasema kuwa kama sio soka ndoto yake ilikuwa ni kuwa Daktari.

KIPA HADI KIUNGO Sio kila mchezaji anaweza kucheza nafasi zote uwanjani japo kuna wachezaji kama hao wapo na kuna wengine mbali na kuwa mafundi kwenye nafasi wanazocheza wamebadilishwa namba na makocha.

“Nikiwa nacheza cha ndimu mipira ya makaratasi nilikuwa nakaa golini ‘kipa’ na nilikuwa mzuri sana eneo hilo kutokana na urefu wangu lakini kadri umri ulivyokuwa unasonga nikabadilika.

“Naweza kucheza juu namba nane na chini kiungo mkabaji ni nafasi ambazo nafurahia kucheza hakuna kocha aliyenibadili nafasi ni mimi mwenyewe nilikuwa nasogea nafasi na kujikuta nikicheza nafasi hii ninayocheza sasa,” anasema Andambwile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: