Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simu ya Mudathir imepatikana, Yanga yaikanda Kagera

Mudathir Guede Aziz Ki A0008 Wachezaji wa Yanga wakishangilia

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikiwa zimesalia dakika saba kabla ya mchezo kumalizika, kiungo Mudathir Yahya aliyetokea benchi amefanikiwa kupeleka kicheko mitaa ya Jangwani kutokana na kufunga goli pekee lililoipa ushindi timu ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar.

Goli alilofunga Mudathir (Mfalme wa Chamazi) dakika ya 83, limetokana na pasi ya Stephane Aziz Ki, huku kiungo huyo akiwa ana dakika 11 tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Pacome Zouzoua.

Hiyo ilikuwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ambapo ilishuhudiwa kipindi cha kwanza kilimalizika kwa matokeo ya 0-0.

Mabadiliko kadhaa ya kipindi cha pili ndiyo yaliamua mchezo huo na kuzipata pointi tatu muhimu uwanja wa nyumbani baada ya mzunguko wa kwanza ugenini kutoka 0-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Ushindi huo ni muendelezo wa kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC ambapo sasa tumefikisha pointi 68 baada ya kushuka dimbani mara 26.

Zimesalia mechi nne kabla ya msimu kumalizika ambapo tunahitaji pointi tano pekee kutetea ubingwa wetu.

Katika mechi nne zilizosalia tutacheza dhidi ya Mtibwa Sugar (ugenini), Dodoma Jiji (ugenini), Tabora United (nyumbani) na Tanzania Prisons (nyumbani).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live