Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simu moja ya Terry ilivyobadili maisha ya A-Star

Alsanawii Simu moja ya Terry ilivyobadili maisha ya A-Star

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ahmed Alsanawi almaarufu kama A-Star ni Kinyozi maarufu sana kati ya Wanasoka mahiri wa Kimataifa.

Baadhi ya wateja wake ni kama Eden Hazard, Jack Grealish , Erling Haaland, Paul Pogba na Kylian Mbappe.

Pembeni ya kuwa na salon yake, Kinyozi huyo husafiri katika maeneo na nchi mbalimbali kutoa huduma kwa wachezaji haswa kwenye timu nzima katika mashindano makubwa kama Kombe la Dunia n.k

Alsanawi (32), ameuchukua ulimwengi wa Vinyozi kwa nguvu kubwa, Kijana huyo alikuwa haongei hata neno moja la Kiingereza alipokuwa anahamia Uingereza akitokea Baghdad, Iraq akiwa na umri wa miaka 9.

Saluni yake iitwayo A Star Barbers ilifunguliwa rasmi mwaka 2013, huko Chessington , Uingereza na kila leo himaya yake ya biashara inazidi kuongezeka.

Saluni hiyo ilikuwa kwenye eneo ambalo Wanasoka kadhaa huko Chelsea wakiwemo vijana wa Academy walikuwa wakipita kukatwa nywele baada ya mazoezi.

”Ilikuwa ni simu moja ya John Terry iliyobadili maisha yangu. Vijana wake walihitaji kinyozi mpya, hivyo nilianza kwenda kila Alhamisi mara zingine mara mbili kwa wiki kuwanyoa nywele kina Hazard, Diego Costa, Ces Fabregas na wenzao."

Katika kazi zake za ajabu zaidi anazozikumbuka ni pale alipolazimika kuubadilisha muonekano wa Jose Mourinho masaa machache baada ya kufukuzwa kazi Chelsea.

”Ilibidi nimnyoe nywele zote mana hakutaka kujulikana, alitokea mlango wa nyuma kutoka uwanja wa mazoezi, nilikosa la kusema”

Miaka kumi ya biashara hii ukurasa wa Instagram wa A-Star una wafuasi milioni 1.1. Alsanawi anasema yuko ‘busy’ na kazi ni nyingi sana. Hivi sasa kijana huyo amewekeza pia kwenye nyumba , mgahawa na biashara zingine.

Ikiwa unafikiria siku moja kunyolewa nywele na Alsanawi ujumbe wake ni mmoja tu ”sitomgusa mtu yoyote kwa pesa ndogo”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live