Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simone Inzaghi: Haikuwa rahisi, lakini imewezekana

WhatsApp Image 2024 04 23 At 11.jpeg Simone Inzaghi: Haikuwa rahisi, lakini imewezekana

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: Dar24

Baada ya kuiwezesha Inter Milan kutwaa Ubingwa wa 20 wa Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’ Kocha Mkuu wa klabu hiyo Simone Inzaghi ameelezea furaha yake, kufuatia mafanikio hayo msimu huu 2023/24.

Inter Milan ilijihakikishia Ubingwa wa ‘Serie A’ usiku wa kuamkia leo Jumanne (Aprili 23) kwa kuichapa AC Milan 2-1, na kufanikiwa kufikisha alama 86, wakiwaacha wapinzani wao hao kutoka jijini Milan na alama 68.

Mabao ya Inter Milan katika mchezo huo yalikwamishwa wavuni na Francesco Acerbi na Marcus Thuram, huku Fikoyo Tomori akifunga bao la kufutia machozi kwa AC Milan.

Kocha Inzaghi amesema imekuwa furaha kwake, kwa sababu amekuwa na mipango na mikakati ya kuutaka Ubingwa wa ‘Sirie A’ tangu mwanzoni mwa msimu huu, hivyo hana budi kumshukuru Mungu kwa kumfanikishiA hilo usiku wa kuamkia leo Jumanne (Aprili 23).

Amesema aliwahimiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma wakati wote, hawakuidharau timu yoyote na walitimiza wajibu wao katika kila dakika ya kila mchezo, hivyo ilikuwa rahisi kwao kufanikisha walichokipanga tangu mwanzoni mwa msimu huu.

“Ni mhemko wa kushangaza, tulifanya jambo la kushangaza na ni sawa kushiriki na watu wengi iwezekanavyo,” amesema Inzaghi akiiambia DAZN.

“Kuna wahusika wakuu wengi wa mafanikio haya, kwanza kabisa wachezaji, lakini pia wakurugenzi na Rais Steven Zhang, kwani chochote tulichohitaji katika safari hii kilitolewa kwa ajili yetu.

“Ni wazi, mawazo yangu pia yanaenda kwa familia yangu, mke wangu Gaia, watoto wangu, wazazi wangu. Kizuizi changu ni kwamba mara nyingi siwezi kuacha kazi yangu kazini na huwa na kurudi nayo nyumbani, lakini zilikuwa za msingi kwangu.”

“Ulikuwa mchezo mzuri dhidi ya AC Milan, inasikitisha kwamba ilikuwa na mvutano katika dakika tano za mwisho, kwani ilikuwa ya haki hadi wakati huo. Tulicheza vizuri, tungeweza kufunga bao lingine katika kipindi cha kwanza, lakini tuna furaha sana.

“Ilikuwa safari ndefu kwangu na wafanyikazi wangu. Unafanya kazi kila siku kujaribu kuboresha. Nikikumbuka mechi zangu za kwanza za Ligi ya Mabingwa hapa nikiwa na Real Madrid na Liverpool, ambao walikwenda Fainali mwaka huo, tayari ningeweza kuona dalili chanya na nilikuwa na imani kwamba tunaweza kuendeleza hilo ili kuendelea na kutwaa mataji sita. ” amesema Inzaghi

Chanzo: Dar24