Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simon Patrick awapiga dongo Simba

Mangungu Mo Dewji Simon Patrick awapiga dongo Simba

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Sheria na Mashabiki wa Klabu ya Yanga, Wakili Simon Patrick amewapiga dongo watani zao wa jadi, Klabu ya Simba baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu huu.

Mambo 5 ya kufungia msimu yanayotufurahisha wananchi;

1. Wakitaka kusema tumezionea timu dhaifu msimu huu unakuta timu yao tumeikanda goli 7 na kukusanya point 6.

2. Wakitaka kumlinganisha Aziz Ki na mchezaji waliotaka awe mfungaji bora, unakuta Aziz Ki ndiye kinara wa magoli na kawakanda mechi zote.

3. Wakitaka kujiita wajuaji wa mechi za kimataifa unakuta timu yao haitashiriki klabu bingwa msimu ujao.

4. Wakitaka kusema mafanikio yao msimu huu unakuta wana WhatsApp channel na kibegi kama mafanikio.

5. Wakitaka kusema Mzee awaachie timu yao wanakuta timu ishanunuliwa kitambo kwa mujibu wa taarifa ya mnunuzi. Kwa ufupi timu yao imefeli vita zote msimu huu, vita ya ubingwa, vita ya nafasi ya pili na vita ya mchezaji wampendao kutwaa kiatu cha ufungaji bora.

NB: Muda wa kutumia ile 20B umefika sasa Manzoki aje kuokoa jahazi laa sivo mtaendela kuteka wachezaji Airport.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live