Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simkoko apewa mikoba Ihefu

Simkoko Ihefu.jpeg Simkoko apewa mikoba Ihefu

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Ihefu inayosjiriki Ligi Kuu Bara imetangaza kufikia makubaliano na John Simkoko kuwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kuanzia leo Februari 12, 2023.

Simkoko amechukua nafasi ya Juma Mwambusi aliyekwa akishika nafasi hiyo tangu mwezi Septemba mwaka jana.

Taarifa ya Ihefu imeeleza kuwa Simkoko ataungana na benchi la ufundi lililopo kikosini hapo ili kufanikisha malengo yake.

Baada ya Mwambusi kuondoka kikosini hapo, Ihefu ilikuwa chini ya kocha Zuberi Katwila ambaye ni msimu wake watatu ndani ya matajiri hao wa Mbeya.

Katwila alijiunga na Ihefu katikati ya Msimu wa 2020/2021, na kushindwa kuinusuru kushuka daraja, akaiongoza kwenye Ligi ya Championship msimu uliopita na kuipandisha tena Ligi Kuu msimu huu.

Simkoko ni mzoefu wa soka la Tanzania akiwa na rekodi ya kuipa Mtibwa Sugar ubingwa wa ligi mwaka 2000.

Aidha amewahi kuzinoa timu nyingine mbalimbali za Ligi Kuu ikiwemo KMC na Polisi Tanzania. Ihefu sasa ipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 22, kushinda nane, sare mbili, na kupoteza 12 ikivuna alama 26 na leo kuanzia saa 10:00 jioni itakuwa iwanjani ikicheza mchezo wake wa 23 kwenye ligi dhidi ya Singida Big Stars iliyo nafasi ya nne na pointi 43.

Chanzo: Mwanaspoti