Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simeone akili yote kwa Real Madrid

Diego Simeoneeeee Atl Diego Simeone

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amesema kuwa mzozo uliopo kati yao na wapinzani wao Real Madrid ni “Filamu Mpya” huku akisisitiza kuwa hali hiyo haina maana yoyote kuelekea mchezo wao wa Derby unaotarajiwa kupigwa Jumapili.

Simeone anawakabili vijana wa Carlo Ancelotti ambao wamekuwa na kiwango bora toka kuanza kwa msimu huu huku Atletico wakiwa wametoka kupoteza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Liverkusen.

Simeone amethibitisha kuwa mlinda mlango wake Oblak atakuwa fiti kuanza baada ya kupata ahueni baada ya kupata jeraha siku chache zilizopita ambapo amesema kuwa mchezo wa kwanza kati yao utawakilisha mwanzo mpya kwa timu hizo mbili.

Simeone: "Tutakutana na Timu Kubwa Yenye Wachezaji Wazuri"

Simeone alisema kwamba; “Siku zote huwa nafikiri kwamba katika michezo mikubwa na kwenye Derby, ni muhimu jinsi unavyofika,” Aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi. ” Ningependa kuja na ushindi na kuangalia kila mara kutoka upande chanya”

Aliendelea kusema kuwa kila mchezo unapoanza ni hadithi mpya. Kila kitu ni kizuri sana hadi mwamuzi aanze; ni filamu mpya ambayo hatujui mwisho wake, ndiyo maana mchezo huu unafurahisha sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live