Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simeone: Tunahamishia Nguvu Michuano ya Europa

Ds Diego Simeone

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Atletico, Madrid Diego Simeone amekiri kuwa timu yake bado wanaumia sana kutokana na kuondoka kwao mapema Ligi ya Mabingwa lakini ameapa kupambana kwa nguvu ili aweze kufuzu kwenye Ligi ya Europa.

Atletico ilishindwa kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo mikubwa ya vilabu barani Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano baada ya kutoka sare ya 2-2 nyumbani dhidi ya Bayer Leverkusen wiki iliyopita, ambapo Yannick Carrasco alikosa penalti ya dakika za mwisho.

Kikosi cha Simeone pia kinazidiwa pointi 9 dhidi ya Real Madrid huku wakiwa hawajashinda katika mechi zao nne zilizopita za Ligi ya Mabingwa, ikiwa ni muda mrefu zaidi tangu Desemba 2008 na Desemba 2009.

Atletico walishindwa kushinda katika mechi tisa katika kipindi hicho kabla ya kuteuliwa kwa Simeone, ambaye alikiri yeye na wachezaji wake bado wana wasiwasi wa kuondolewa kabla ya pambano la Jumanne dhidi ya Porto.

“Leo tumetoka kwenye Ligi ya Mabingwa. Inatuumiza, inaniacha na maumivu kwa sababu ya jukumu tulilonalo na watu wengi wanaokua katika klabu, Lakini ni ukweli na hatuwezi kwenda kinyume. Ukweli ndio tulionao na kuona kama tunaweza kueleza kile tunachohisi uwanjani.

Simeone amesema kuwa yupo tayari kushindana na hajui jinsi ya kufanya hivyo kwa njia nyingine yoyote akijua kwamba anaweza kupoteza lakini ni bora kushinda na malengo yake ni Europa huku akiangalia nafasi aliyopo kwenye Kundi hilo B.

Wataingia uwanjani wakijua kwamba wana mechi ngumu mbele yao na timu bora, na wanajua kwamba hawako kwenye Ligi ya Mabingwa lakini ni Ligi ya Europa na ni muhimu sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live