Kutokana na hali ya hewa kuwa rafiki nchini Morocco, uongozi wa Simba umeahidi kutoruhusu tena kufungwa na Raja Casablanca katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikumbukwe katika mchezoo wao wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Simba ilipigwa mabao 3-0 na sasa inataka kwenda kulipiza kisasi huko Morocco.
Akizungumza nasi, Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema, wanamshukuru Mungu kuona hali ya hewa ya Casablanca siyo baridi sana jambo ambalo ni faida kwao kupambana kulinda heshima kwenye mchezo huo.
“Tunamshukuru Mungu tayari wachezaji wote waliotangulia wamewasili salama, hivyo wamefanya mazoezi mepesi hivyo kufutia uwepo wa baridi ya kawaida hatutaruhusu kufungwa tena na Raja CA na badala yake tumekuja kulinda heshima yetu baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya Horoya AC (walishinda mabao 7-0).
“Wachezaji wote waliokuwa timu za taifa nao tayari wapo kwenye maandalizi ya mchezo wetu huo utakaopigwa Machi 31,” alisema Abbas.
MATOKEO YA SIMBA CAF
Horoya 1-0 Simba
Simba 0-3 Raja
Vipers 0-1 Simba
Simba 1-0 Vipers
Simba 7-0 Horoya
Raja vs Simba?