Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yawafuata Nkana, mwendo uleule!

31353 PIC+SIMBA TanzaniaWeb

Wed, 12 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kikosi cha Simba kimeondoka nchini leo Jumatano alfajiri kwenda nchini Zambia ambako itacheza mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana Desemba 15.

Ukurasa wa Insatgram wa klabu hiyo iliweka picha  na maelezo yakionyesha wachezaji wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Zambia.

Simba ilifanikiwa kuvuka hatua hii ya awali baada ya  kuiachia maumivu Mbabane Swallows  mabao 4-1 kisha kuwaondoa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 8-1.

Mashabiki wa klabu hiyo kupitia mtandao wa klabu yao waliandika ujumbe wakiitakia kila heri timu yao ipate ushindi kwenye mchezo huo muhimu.

Pia baadhi ya mashabiki waliandika kwenye ukurasa huo wa Instagram wakiusihi uongozi wa klabu yao kuangalia namna ya kuboresha mavazi ya wachezaji wao wanapokuwa safarini ili wawe nadhifu zaidi.



Chanzo: mwananchi.co.tz