Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatumia dakika moja kumkumbuka Gembe

Simba SC X GEMBE Simba yatumia dakika moja kumkumbuka Gembe

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Simba imetumia dakika moja kuomboleza kifo cha aliyekuwa daktari wao, Yassin Gembe aliyefariki jana katika Hospitali ya taifa Muhimbili.

Simba imetumia muda huo wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya AS Arta Solar 7 ya Djibouti unaoendelea katika Uwanja wa Uhuru.

Mwamuzi wa mechi, Ramadhan Kayoko kutoka Dar es Salaam alisimamisha mchezo huo ili kutoa nafasi ya kuomboleza kifo hicho kilichogusa mioyo ya mashabiki wengi wapenda soka.

Gembe ambaye aliwahi kufanya kazi katika klabu ya Mtibwa Sugar kabla ya umauti kumfika alikuwa daktari wa timu ya vijana Simba (Youth Team) huku pia akiwahi kufanya kazi na timu ya wakubwa (Senior Team).

Simba inacheza mchezo huu wa tatu kwake wa kirafiki baada ya kucheza na Asante Kotoko ya Ghana na kushinda mabao 4-2 Agosti 28, kisha kufungwa bao 1-0 na Al Hilal ya Sudan Agosti 31, katika mashindano maalumu yaliyofanyika Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live