Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatua kwa mrithi wa Ayoub Lakred

John Noble John Noble

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi za usajili zinaeleza kuwa, Klabu ya Simba iko katika mazungumzo na golikipa wa Tabora United, John Noble ili kuchukua nafasi ya kipa wao anayetajwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Ayoub Lakred amekuwa kwenye kiwango bora sana kwa sasa huku akiwabeba wekundu hao wa msimbazi lakini ameshitua Kwa kuwaambia kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapomalizika.

Taarifa zinaeleza kwamba, Simba wanamuona Noble kuwa kipa sahihi wa kuidakia timu hiyo kwani ni golikipa mwenye uwezo wa juu akiwahi kuichezea klabu ya Enyimba na timu ya Taifa ya Nigeria.

Kabla ya kumsajili Lakred, klabu ya Simba ilikuwa ikimuwinda kipa huyo kabla ya kuzidiwa kete na Tabora United. Hata alipotua nchini, Simba walijaribu kumsajili ili kuipiku Tabora jambo ambalo liliwazindua viongozi wa Tabora na kumsainisha mkataba haraka.

John Noble alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Tabora United hivyo haitakuwa shida Kwa Simba kumpata na pia mchezaji huyo hawezi kukataa fursa ya kuitumikia klabu hiyo inayoshiriki michuano ya vilabu barani Afrika mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live