Mabingwa watetezi, Simba SC wametoa onyo kali baada ya kuitandika KMC mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na mabeki, Mohamed Hussein ‘ Tshabalala’, dakika ya 10, Mkenya Joash Onyango dakika ya 12 na mshambuliaji Kibu Dennis mawili dakika ya 46 na 56, wakati la KMC limefungwa na Abdul Hillary dakika ya 41.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi tisa.
KMC yenyewe inabaki na pointi zake 10 katika nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi 10 sasa.