Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatoa zawadi ya Krismas CCM Kirumba

Henock Inonga Baka Kirumba.jpeg Mfungaji wa bao la tatu la Simba, Henock Inonga akishangilia

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi, Timu ya Simba SC imekusanya alama tatu na magoli matatu mbele ya watoza ushuru wa Manispaa ya Kinondoni, Timu ya KMC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mchezo huo wa raundi ya 18, umewashuhudia Simba wakiingia kwa kasi wakisaka alama 3 ili kupunguza pengo la alama baina yao na Vinara Yanga.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa nahodha John Bocco aliemalizia krosi safi ya Shomari Kapombe dakika ya 16.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Simba walienda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa uongozi wa bao 1-0.

Kipindi cha pili KMC waliingia kwa kasi na kufanya mashambulizi langoni kwa Simba na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Sadala Lipagile dakika ya 52.

Augustine Okrah akairudisha Simba katika uongozi kwa bao lake kali baada ya kutokea piga nikupige katika lango la KMC.

Henock Inonga Baka akamalizia kazi kwa kupiga bao safi la kichwa na kuwapa Simba uhakika wa kuondoka na alama tatu.

Kwa ushindi huo Simba inafikisha alama 41 katika nafasi ya pili wakiwa na tofauti ya alama 6 dhidi ya vinara Yanga wenye alama 47 huku wote wakiwa wameshashuka dimbani michezo 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live