Klabu ya Coastal Union imerudisha fedha ambazo Simba SC walikuwa wamelipa kwaajili ya uhamisho wa beki wa kati Lameck Lawi.
Coastal wamethibitisha kufuta dili hilo wakidai Simba imekiuka makubaliano ambayo yapo kinyume na utaratibu.
Simba yatoa tamko;
“Ndio tulichelewa kumaliza pesa, tulilipa nusu lakini mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yoye ya usajili.
"Tumemsajili Lameck Lawi kwa kufuata utaratibu. Wangesema kama ukichelewa kulipa mkataba unavunjika. Mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yote na nyaraka zote tunazo hata tukienda FIFA lakini Kilichotokea ni Coastal Union wakapata deal kutoka nje ndio maana wakabadili maamuzi.
"Tunafanya kazi kiweledi sana. Hoja yao ni dhaifu. Hoja yao pesa iwe imelipwa yote na kusema hawatambui mkataba. Mpira ni wa FIFA na hauishii hapa. Kiukweli hii imetusumbua na tutakabiliana nalo. Simba SC tumefuata taratibu zote za kumsajili Lameck Lawi,“ amesema Mjumbe wa Bodi ya Simba, Cresentius Magori.