Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatoa neno usajili wa Miquissone, Manzoki

Luis Miquissone 1 680x454 1 Miquissone

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba umesema wanafurahi kuona wanahusishwa na usajili wa wachezaji Luis Miquissone na Cesar Manzoki katika kipindi hiki cha dirisha dogo na kuongeza watakapokamilisha mchakato huo watawatangazia mashabiki wao.

Miquissone anayekipiga katika klabu ya Al Ahly ya Misri ambayo inahitaji kumtoa kwa mkopo na Manzoki akiicheza DL Pro inayoshiriki Ligi Kuu ya China, wamehusishwa zaidi na Simba wakati dirisha dogo likiwa limefunguliwa.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema wanafanya usajili mzuri na wanaenda kununua mikataba ya wachezaji wakubwa ambao wanawahitaji.

Alisema kuhusu Miquissone na Manzoki ni wachezaji wazuri na kulingana na uwezo wao hakuna timu isiyohitaji huduma za nyota hao ila wanaheshimu mikataba yao.

"Hao wachezaji wana mikataba na klabu zao, tunaheshimu sana na kama itakuwa wako katika mipango yetu basi tutalazimika kufanya nao mazungumzo na hizo klabu ila kwa sasa tunaheshimu mikataba yao," alisema Ahmed.

Aliongeza mapendekezo waliyopokea kutoka katika benchi la ufundi lililoko chini ya Juma Mgunda, watayafanyia kazi kwa kuwanasa wote wanaolengwa iwe kwa kutumia dau kubwa au kuvunja mikataba waliyokuwa nayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live