Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatoa msaada Hanang

Simba Yatoa Msaada Hanang Simba yatoa msaada Hanang

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba leo imekabidhi msaada kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko na maporomoko Hanang, Manyara ambapo misaada hiyo imepokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ambaye amishukuru klabu ya Simba kwa kutoa msaada huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Try Again amesema, “Kwa niaba ya Rais wa heshima Mo Dewji, Bodi, Uongozi, Wapenzi na Wanachama wa Simba tunapenda kutoa pole nyingi kwa Wahanga wa mafuriko na maporomoko huko Hanang, wengi wa Wahanga hawa ni Wapenzi wa soka, na sisi kama klabu tunaungana nao kwenye kipindi hiki kigumu”

Tukio hilo limehudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT), Neema Msika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live