Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatinga robo fainali kwa kishindo

Dac20a57fadeda6a1b1cf5a7775de69c Simba yatinga robo fainali kwa kishindo

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba, imeingia hatua ya robo fainali kwa kishindo baada ya kuifurusha AS Vita kwa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo mnono, Simba wamejihakikishia nafasi ya kumaliza wa kwanza katika Kundi A baada ya mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri kutoka sare ya 2-2 na Al-Merrikh Sporting Club ya Sudan jana.

Kwa matokeo hayo ya jana, Simba ambayo hadi sasa haijafugwa mchezo wowote na imeruhusa bao moja tu, imefikisha pointi 13, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya kundi hilo hata kama itafungwa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Al Ahly kwao.

Mchezo huo wa Simba ulianza kwa kasi huku AS Vita walikuwa wa kwanza kufika katika lango la Simba, katika dakika ya sita kupitia kwa Jaques Mangoma, Simba walijibu mapigo dakika ya 11 kupitia kwa Clatous Chama, ambaye shuti lake lilienda nje ya lango.

Simba walirudi tena katika lango la AS Vita dakika ya 12, kupitia kwa shuti kali la Luis Miquissone lililoenda nje wenyeji waliendelea kuliandama lango la AS Vita na katika dakika ya 16, Chris Mugalu kichwa chake kilienda nje ya uwanja dakika 17, Simba walirudi lakini shuti la Morrison lilienda nje ya lango.

AS Vita walirudi kwa kasi dakika ya 25 ambapo shuti la Moloko liliokolewa na kipa Aishi Manula na kuwa kona ambayo iliokolewa katikati ya mstari na Mohamed Hussein, wenyeji waliandika bao la kwanza katika dakika 30 kupitia kwa Luis Miquissone akimalizia vyema pasi ya Benard Morrison,

Hatahivyo, bao hilo halikudumu kwani Vita walisawazisha katika dakika ya 31 kupitia kwa Semanga Soze kwa shuti kali na mpira kugonga mwamba na kujaa wavuni na kumuacha Manula akishangaa.

Simba walirudi kwa kasi katika dakika 35, ambapo Chris Mugalu, alikosa bao la wazi akiwa yeye na kipa Simon Omosola, dakika ya 36,

Wenyeji Simba ambao walicheza vizuri walipata bao la pili katika dakika ya 44 kupitia kwa Clatous Chama akimalizia pasi ya Mohamed Hussein.

Hadi kipindi cha kwanza kinaisha Simba walikuwa mbele kwa bao 2-1, kipindi cha pili kilianza kwa Vita kufanya mabadiliko ya kumtoa Fiston Mayele na kuingia Kabwe iliwachukua dakika 48 Simba, kulifikia lango lakini mpira wa Chama ulienda juu ya lango licha ya kuwa mbele wenyeji waliendelea kuliandama dakika 49 Benard Morrison na Ousmane Ouatara wanaonyeshwa kadi ya njano.

Simba walifanya mabadiliko katika dakika ya 60, wakimtoa Morrison na kuingia Larry Bwalya, wakimtoa Mugalu na nafasi yake kuhukuliwa na Meddie Kagere.

Wenyeji walipata bao jingine katika dakika ya dakika ya 65 kupitia kwa Bwalya akimalizia pasi ya Chama, licha ya kupata bao hilo Simba waliendelea kuliandama lango la AS Vita ambapo dakika ya 70 Chama nusura afunge.

Chama anasahihisha makosa yake kwa kufunga bao la nne katika dakika ya 83 akimalizia pasi ya Miquissone.

Simba walifanya mabadiliko katika dakika ya 86 kwa kuwatoa Miquissone na Chama na kuwaingiza Francis Kahata na Hassan Dilunga, hadi dakika 90 zinamalizika Simba wanafuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara wa Kundi A kwa kujikusanyia pointi 13.

Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Shomary Kikombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Serge Paschal Wawa , Thadeo Lwanga, Luis Miquissone, Jonas Mkude , Chris Mugalu, Clatous Chama na Benard Morrison.

Chanzo: www.habarileo.co.tz