Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatinga robo fainali CAFCL kibabe, yaishindilia Jwaneng bao 6-0

Simba Robo Sm Simba yatinga robo fainali CAFCL kibabe, yaishindilia Jwaneng bao 6-0

Sat, 2 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC kwa mara nyingine imefanikiwa kutinga kwa kishindo hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kuwakanda Jwaneng Galaxy ya Botswana 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.

Kabla ya mchezo huo kocha mkuu wa Jwaneng Galaxy alinukuliwa akiitambia Simba SC kwa kusema kuwa kikosi hicho kimejaa wazee na kama wanataka kisasi waanze kwanza kulipa kipigo cha bao 5-1 walichokipata kwa Yanga.

Timu ya Simba imemaliza Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata ushindi mnono wa magoli 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam

Waliocheka na nyavu katika mchezo huo ni Saidi Ntibazonkiza (7), Pa Omary Jobe (14), Kibu Denis (22), Clatous Chama (76), Ladaki Chasambi (86) na Fabrice Ngoma (89)

Baada ya matokeo hayo, msimamo wa mwisho wa Kundi B, ASEC Mimosas ya Ivory Coast imeongoza kwa kuwa na pointi 11, Simba ina 9 sawa na Wydad AC ya Morocco huku Jwaneng ikiwa na alama 4

Hii ni mara ya kwanza kwa timu mbili za Tanzania kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya Yanga SC kufuzu mapema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live