Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatinga bungeni na tambo

Dee41bb303db6dc7239b91c3261421a5 Simba yatinga bungeni na tambo

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wametinga jana bungeni huku Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez akitamba timu hiyo kuchukua ubingwa wa mpira wa miguu barani Afrika.

Mabingwa hao walitambulishwa bungeni katika kipindi cha maswali na majibu na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Dk Tulia alisema ugeni huo una watu 34 ambao ni wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa timu Gonzalez pamoja na Msemaji wa timu hiyo Haji Manara.

Kutokana na shangwe za wabunge hao, Dk Tulia alilazimika kuwasimamisha kwa muda ili kukamilisha matangazo ya Bunge.

Akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge, Gonzalez alitamba timu hiyo kuchukua ubingwa wa mpira wa miguu barani Afrika.

Alisema Simba ina malengo makubwa kimataifa hasa kuwa mabingwa wa michuano ya ndani na ile ya kimataifa.

Timu hiyo leo itaanza kuvitumikia viporo vyake vya Ligi Kuu kwa kucheza dhidi ya Dodoma Jiji katika Uwanja wa Jamhuri hapa.

Chanzo: habarileo.co.tz