Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatinga 2022 kibabe, Sakho mtu hatari

Sakho Danger Mfungaji wa goli la pili la Simba, Pape Ousmane Sakho

Sat, 1 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye kitendawili cha nani mbabe kimepata jibu katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam baada ya Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1, baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika bila kuona goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam kufanya mabadiliko baada ya kumtoa Charles Zulu na nafasi yake kuchukuliwa na Tepsie Evance.

Mabadiliko hayo yalionekana kuleta tija kwa upande wa Azam ambao walikuwa wanategemea mashambulizi ya kushitukiza kupitia kwa Tepsie Evance na Ismail Aziz Kader.

Dakika ya 58, Azam iliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Mudathir Yahaya, Idris Mbombo huku nafasi zao zikichukuliwa na Shaban Iddy Chilunda na Rodgers Kola.

Dakika 66, Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Meddie Kagere, Larry Bwalya huku nafasi zao zikichukuliwa na Mzamiru Yassin na Chris Mugalu.

Dakika ya 67, Simba ilipata bao la utangulizi kupitia kwa Sadio Kanoute aliyepiga kichwa safi baada ya Friikiki iliyopigwa na Mohamed Hussein 'Tshabalala'

Simba ilipata bao la pili dakika ya 72, kupitia kwa Pape Ousmane Sakho baada ya mabeki wa Azam Daniel Amoah na Abdallah Kheri kumsindikiza kwa macho kufuatia pasi safi iliyopigwa na Kibu Denis.

Azam ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Rodgers Kola dakika ya 80, kufuatia krosi iliyopigwa na Tepsie Evance.

Katika michezo 11, iliyopita ambapo timu hizo zimekutana Simba imeshinda sita, sare nne, huku Azam FC ikishinda mchezo mmoja tu.

Huu ni mchezo wa 27, kwa timu hizi kukutana kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ambapo Azam imeshinda mitano, sare tisa na kupoteza 13.

Matokeo haya yanaifanya Simba kufikisha pointi 24, ikiwa nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 29, baada ya michezo 10, wakati Azam FC inashika nafasi ya saba na pointi 15, baada ya kucheza michezo 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live