Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatia Timu Berkane, Kila mtu yuko fiti

Simba Berkane Msafara wa Kikosi cha Simba ukiwasili Berkane

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba Kimewasili Salama katika mji wa Berkane kutoka Jiji la Casablanca tayari kwa mchezo wao wa Kesho dhidi ya wenyeji RS Berkane mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane saa nne usiku kwa saa za hapa nchini(Tanzania).

Baada ya kufika kikosi cha Simba kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane majira ya saa nne usiku, muda ambao ndio utakaopigwa mchezo siku ya kesho.

Mpaka sasa Sima SC ndio Kinara katika kundi D akiwa anaongoza kwa alama 4, huku wanaomfuata ASEC Mimosas na RS Berkane wana alama tatu na USGN wana ala 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live