Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yategua mtego

Pic Data Simba yategua mtego

Wed, 3 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

SIMBA inapaa kesho kuwafuata El Merreikh ya Sudan katika mchezo wao wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, huku kocha wa Wekundu hao, Didier Gomes, akisema: “Tulieni nawafahamu vizuri hawa.“

Gomes ambaye ameiongoza Simba katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa walizoshinda kibabe ugenini dhidi ya AS Vita na nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, amesema mechi itakuwa ngumu lakini ushindi ndio lengo namba moja.

“Tunakwenda kucheza na timu ambayo naifahamu vizuri, tumeandaa mbinu nyingi za kwenda kukabiliana nao ili kuhakikisha tunapata pointi nyingine ugenini ingawa tunatambua si jambo rahisi,” alisema na kuongeza:

“Tumefanya maandalizi ya kutosha kulingana na ambavyo tumewaona wapinzani wetu. Tutatumia udhaifu wao kuwazidi ili kufanya vizuri na ninaamini itakuwa hivyo.

“Wamepoteza mechi mbili, moja nyumbani kwao na nyingine ugenini, hili litaongeza ugumu wa mechi yetu, watataka kupata ushindi wa kwanza, tupo tayari kwa hilo na tutapambana nao,” alisema kocha huyo Mfaransa.

Simba inahakikisha hainasi katika mtego wowote utakaowavurugia mipango yao ya kupata pointi tatu ugenini hivyo imetanguliza jeshi la kwenda kuchonga njia kabla ya timu haijatua mjini Omdurman kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa wikiendi hii.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz