Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatanguliza mguu mmoja, hatua ya makundi Klabu Bingwa

Simba Mchezo Botswana Matokeo ya Mchezo wa Jwaneng Galaxy dhidi ya Simba

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa nchi, Klabu ya Simba, imeibuka na ushindi mnono wa magoli 2-0 huko ugenini nchini Botswana, katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa hatua ya Makundi klabu bingwa Afrika.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Taifa wa Botswana umewashuhudia Simba wakijipatia magoli ya haraka haraka ndani ya dakika 5 za kwanza , magoli yaliyowekwa kimiani na kiungo Mganda Taddeo Lwanga 2' na Nahodha John Bocco 5'.

Magoli hayo yamedumu mpaka zunakamilika dakika 90, na hivyo Jwaneng Galaxy watakua na kibarua kizito cha kupindua matokeo katika mchezo wa marudiano kwa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Simba imewakosa wachezaji wake nyota kadhaa akiwemo Straika Chriss Mugalu.

Mchezo wa marudiano baina ya Simba na Jwaneng Galaxy utapigwa Oktoba 24 kwa Mkapa Dar es Salaam

Chanzo: www.tanzaniaweb.live