Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatangaza kamati ya uchaguzi

Bodi Simba SC 1140x640 Simba yatangaza kamati ya uchaguzi

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba imefanya uteuzi wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo ambayo itahusika na kuandaa na kusimamia uchaguzi mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Mh. Boniface Lihamwike akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Wakili Mwajuma Choggy pamoja na wajumbe watatu ambao ni Richard Mwalibwa, Gerald Mongela pamoja na Juma Simba.

Kwa mujibu wa taarifa ilyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba kupitia kurasa rasmi ya mtandao wa kijamii wa Instagram imebainisha kuwa wateule hao wataanza kazi mara moja baada ya uteuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live