Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatambulisha kocha mpya

HITIMANA Kocha msaidizi wa Simba, Thierry Hitimana

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imemteua aliyewahi kuwa kocha wa Namungo FC Thierry Hitimana (42) kutoka burundi kuwa kocha msaidizi wa Simba.

Kabla ya Hitimana, kocha msaidizi wa Simba alikua ni nahodha wa zamani wa Simba na kocha wa zamani wa Lipuli Selemani Matola.

“Tunajipanga kufika mbali zaidi kwenye michuano ya mwaka huu kwa kuimarisha benchi la ufundi kwa kumteua Thierry Hitimana kuwa kocha msaidizi wa klabu,” - Imeeleza Taarifa ya Simba iliyotolewa katika mitandao yake ya kijamii.

Wadau wengi wa masuala ya Soka wamesifu usajili wa Kocha Hitimana kwa kudai ana uwezo mkubwa na anaweza kufanya makubwa ndani ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live