Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatakata Chamazi, yaichapa Geita Gold kipigo kizito

Simba Shangwezzz Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kushinda mchezo huo

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Geita Gold FC kwenye muendelezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara

Ushindi huo umeisadia Simba SC kupunguza bao moja kwenye tofauti ya wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa kati yao na Azam FC ambao mapema walipata ushindi muhimu ugenini kwa kuizaba JKT Tanzania 2-0.

Simba sasa wameweka tofauti ya wastani wa mabao 5 na waliofungana nao alama wote wakiwa na alama 63, Azam FC bado kwenye nafasi ya pili na Simba SC wakisalia wa tatu.

FULL TIME

Simba Sc 4️⃣ ➖ 1️⃣ Geita Gold

⚽ 11' Geofrey Julius

⚽ 45 +4' Ntibazonkiza (P)

⚽ 72' Ntibazonkiza

⚽ 86' Chasambi (assist Onana)

⚽ 90+6' Chasambi (assist Mzamiru)

1. YANGA SC — mechi 28 — pointi 71 — magoli +47

2. AZAM FC — mechi 28 — point 63 — magoli +36

3. SIMBA SC — mechi 28 — pointi 63 — magoli +31

Timu hizo zote zimebakiza michezo miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live