Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yataka soka burudani Uwanja wa Taifa

90736 Pic+simba+2 Simba yataka soka burudani Uwanja wa Taifa

Fri, 3 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Yanga wakitamba kuibuka na ushindi kesho katika mechi ya Watani wa Jadi, upande wa pili, Simba umesita kujipa uhakika wa moja kwa moja kuibuka na ushindi huku wakitaka pande zote mbili kucheza soka la kiungwana.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck na nahodha wake John Bocco, wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi hiyo ingawa matokeo ya tofauti yanaweza kutokea lakini ni vyema kuwepo na soka la uungwana.

"Tumepata ushindi katika mechi nne mfululizo hivyo naweza kusema mechi hii imekuja katika wakati muafaka ukizingatia ubora ambao tumekuwa nao.

Hata hivyo tunaingia tukifahamu uzito wa pambano hili na kila mmoja amekuwa akilizungumzia na umuhimu wa kupata ushindi hivyo tumejipanga katika hilo ingawa matarajio hayatakiwi kuwa makubwa kupitiliza.

“Nimecheza mechi nyingi za namna hii na nafahamu faida na umuhimu wa kupata ushindi na tuko tayari kuhakikisha tunatimiza hilo. Tunategemea mechi itakuwa nzuri na ya kiungwana na hakutokuwa na masuala ya kupoteza muda na rafu,"alisema Vandenbroeck.

Kwa upande wake nahodha John Bocco alisema wachezaji wa Simba wanatambua umuhimu wa kushinda mechi hiyo.

"Tumejiandaa kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki wetu na tunawaomba wajitokeze kwa wingi na kutuombea huku wakitupa sapoti.

Tunaamini mechi itakuwa nzuri na kila timu itacheza kiungwana na mashabiki watafurahi," alisema Bocco.

Chanzo: mwananchi.co.tz