Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yashusha Mmalawi

DUNCAN NYONIII Nyota Mpya wa Simba, Duncan Nyoni

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club imemtambulisha MMalawi Duncan Nyoni kama mchezaji mpya wakati huu wakijiandaa na Msimu mpya 2021/2022.

Duncan mwenye uwezo wa kucheza kama winga na pia mshambuliaji anaenda kukata ile kiu na wasi wasi walionao Wanamsimbazi baada ya kuondokewa na Nyota wao wawili waliohusika kwenye mafanikio ya Klabu hiyo msimmu uliopita, Clatous Chama na winger Luis Miquissone.

Kikosi cha wekundu hao kwa sasa kipo nchini Morocco kikijifua kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya.

Mpaka sasa Klabu ya Simba imeshamsajili Peter banda kutoka malawi,Yusufu Mhilu huku wakiahidi na kuwasihi mashabiki kutulia kwani mambo mazuri bado yanakuja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live